Mjumbe wa kudumu wa China UM ataka juhudi zaidi katika kuhimiza suluhisho la nchi mbili katika mgogoro kati ya Israel na Palestina
2022-12-20 09:08:46| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, kuwa suala kati ya Palestina na Israel limekuwa kwenye ajenda ya Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miongo saba. Kila siku ambapo jumuiya ya kimataifa haichukui hatua, ni kutotendea vizuri amani, usaliti wa haki na kukosea kizazi kijacho.

Balozi Zhang ametoa wito kwa pande husika kutekeleza ahadi zao kwa haki na kutaka Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kupiga hatua katika kuhimiza suluhisho la nchi mbili na kuunga mkono watu wa Palestina kurejesha na kutekeleza haki zao zisizoweza kuondolewa, ili kuziwezesha Palestina na Israel kuwa pamoja kwa amani, watu wao kuishi kwa maelewano, na pia kupatikana kwa amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya kati.