Watu kadhaa wauawa katika mashambulizi huko kaskazini mwa Nigeria
2022-12-20 09:08:11| CRI

Watu kadhaa wameuawa katika mashambulizi tofauti dhidi ya vijiji viwili katika jimbo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria.

Ofisa mwandamizi wa usalama katika jimbo hilo Bw. Samuel Aruwan, amesema mashambulizi hayo yalitokea katika vijiji vya Malagum 1 na Sokwong vya eneo la Kaura usiku wa Jumapili iliyopita, ambapo washambulizi wenye bunduki walichoma nyumba na mali za wakazi. Amesema operesheni ya dharura ya usalama imetekelezwa na wanajeshi ikilenga kuwakamata wahalifu, lakini hakutaja idadi kamili ya vifo katika mashambulizi hayo.

Umoja wa Watu wa Kaduna Kusini (SOKAPU) wa baadhi ya makabila kusini mwa Kaduna, umesema katika taarifa yake kuwa miili 38 ya wahanga waliouawa ilipatikana baada ya mashambulizi hayo.