Jeshi la Somalia lawaua wanamgambo 150 wa kundi la al-Shabab
2022-12-20 09:06:46| CRI

 Jeshi la Somalia limesema vikosi vyake vimewaua wanamgambo 150 wa kundi la al-Shabab katika operesheni ya wiki moja iliyofanyika katika mkoa wa MiddleShabelle.

Mkuu wa jeshi hilo Bw. Odowaa Yusuf Rage, amesema kundi hilo lilipata hasara kubwa karibu na mji wa Aden Yabal, ambao ulikuwa ngome ya kundi hilo lakini ulikombolewa hivi karibuni.