Mpango wa mafunzo ya uandishi wa habari wa kimataifa wa BRICS wafunguliwa
2022-12-20 09:05:53| CRI

Awamu ya pili la mpango wa mafunzo ya uandishi wa habari mtandaoni kwa wataalamu wa vyombo vya habari kutoka nchi za BRICS imeanza jana, huku wanafunzi 50 kutoka Brazil, Russia, India, China, Afrika Kusini na nchi nyingine zinazoendelea wakishiriki katika programu ya mafunzo ya miezi mitatu, inayoandaliwa na Shirika la Habari la China Xinhua.

Akihutubia ufunguzi wa programu ya mafunzo kwa njia ya video, Mwenyekiti mtendaji wa Baraza la Vyombo vya Habari vya BRICS na mkuu wa Xinhua Bw. Fu Hua amesema programu hiyo iliyopendekezwa na Rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa 13 wa wakuu wa nchi za BRICS mwezi Septemba 2021, inatarajiwa kuwasaidia wanafunzi kutoka nchi zote kuweka dira ya kimataifa, kuongeza hisia ya ushirikiano, kukuza taaluma na uwezo wao wa uandishi wa habari, pamoja na kugundua na kusimulia hadithi bora zaidi za nchi za BRICS, na kufanya sauti ya nchi za BRICS zinazotoa wito kwa manufaa ya pande zote na maendeleo ya pamoja isikike.