Rais wa China China iko tayari kuimarisha uhusiano na Australia juu ya msingi wa kuheshimiana na kunufaishana
2022-12-21 17:27:56| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametumiana salamu za pongezi na gavana mkuu wa Australia Bw. David Hurley na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Anthony Albanese, katika maadhimisho ya miaka 50 tangu nchi hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibalozi.

Rais Xi amesema, katika miaka 50 iliyopita, China na Australia zimepata maendeleo mengi katika ushirikiano wenye ufanisi wa sekta mbalimbali, yakileta faida halisi kwa watu wa nchi hizo mbili. Amesema China na Australia, zikiwa nchi muhimu za sehemu ya Asia na Pasifiki, ukuaji wenye utulivu na afya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendana na maslahi ya msingi ya watu wa nchi mbili, pia unasaidia kuhimiza amani, utulivu na ustawi wa sehemu ya Asia na Pasifiki na dunia kwa ujumla. Rais Xi pia amesema anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Australia, akipenda kufanya juhudi pamoja na Australia kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 50 kushikilia kanuni za kuheshimiana na kunufaishana, ili kuhimiza maendeleo endelevu ya uhusiano wa kimkakati na pande zote kati ya nchi hizo.

Bw. Hurley amesema, uamuzi wa kihistoria uliofanywa miaka 50 iliyopita umetandika njia ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Australia, ambao pia umeleta ukuaji na fursa kwa nchi hizo mbili. Amesema katika siku za baadaye, Australia itafanya juhudi kufuata hadhi ya uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote, kushikilia moyo wa kuheshimiana na kunufaishana, ili kuendeleza uhusiano wa utulivu na kiujenzi na China.