Rais Xi afanya mazungumzo na rais wa Cote d'Ivoire kwa njia ya simu
2022-12-21 09:18:51| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire.

Rais Xi amesema Cote d'Ivoire ni mshirika muhimu wa ushirikiano wa China barani Afrika, na mwaka kesho pande hizo mbili zitaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yao.

Rais Xi amesema China inaishukuru Cote d'Ivoire kwa kuunga mkono kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kupenda kuendelea kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi ya pamoja, kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao, na kuinua uhusiano huo kwenye ngazi ya juu zaidi.

Rais Ouattara amempongeza Rais Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kuishukuru China kwa uungaji mkono muhimu na mchango wake katika kuhimiza amani na ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali ikiwemo Cote d’Iviore.