Rais Xi asema China na Ujerumani ni washirika wa mazungumzo, maendeleo, ushirikiano na kukabiliana na changamoto za kimataifa kwa pamoja
2022-12-21 09:19:29| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa Ujerumani Bw. Frank-Walter Steinmeier, na kusema nchi hizo mbili zimekuwa washirika wa mazungumzo, maendeleo na ushirikiano, na pia washirika katika kushughulikia changamoto za kimataifa.

Rais Xi alisema mwaka huu nchi hizo mbili zinaadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati yao, na ni mwaka wenye umuhimu mkubwa katika uhusiano wa pande mbili. Amesema pande hizo mbili zinatakiwa kuendelea kuheshimiana na kunufaishana, na bila shaka uhusiano wa pande hizo mbili utasonga mbele.

Rais Xi pia amesema pande mbili zinatakiwa kufanya kazi pamoja kuongoza mwelekeo mzuri wa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, na kutumai kuwa Ujerumani itatoa mchango mkubwa katika kuhimiza uhusiano mzuri kati ya pande hizo mbili.