Makamu wa rais wa Tanzania atoa mwito wa kuhifadhiwa kikamilifu kwa Mto Ruaha Mkuu
2022-12-21 09:17:48| CRI

Makamu wa rais wa Tanzania Philip Mpango amewataka wananchi wote wakiwemo viongozi wa serikali kuhakikisha Mto Ruaha Mkuu unahifadhiwa kikamilifu dhidi ya uharibifu wa mazingira. Bw. Mpango aliwakosoa viongozi wa serikali waliokuwa wakiwalinda wakulima na wafugaji wanaoharibu mazingira ya mto huo kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

Ametoa wito huo alipohutubia kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya uhifadhi uliofanyika mkoani Iringa, ambao walijadili kuhusu umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji nchini Tanzania vinavyokabiliwa na uharibifu unaofanywa na shughuli za kibinadamu.

Mto Ruaha Mkuu wenye eneo la kilomita za mraba 83,970 unakaribia kukauka baada ya wakulima na wafugaji kuharibu mazingira ya sehemu ya chanzo cha mto huo.