Ushirikiano wa uchumi wa kidijitali kati ya China na Afrika wawezesha maendeleo ya kilimo cha kisasa Afrika
2022-12-21 11:16:19| CRI

Heri ya Sikukuu ya Christmas msikilizaji popote pale ulipo. Natumaini uko salama na unasherehekea sikukuu hii kwa amani na furaha tele. Ni wakati mwingine tena tunapokutana katika kipindi hiki cha DARAJA kinachokujia kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti inayohusu ushirikiano wa uchumi wa kidijitali kati ya China na Afrika unavyowezesha maendeleo ya kilimo cha kisasa barani Afrika. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yanayohusu kampuni za China nchini Kenya zimeandaa maonyesho maalum ya siku mbili katika chuo kikuu cha Nairobi, ili kutoa nafasi za ajira kwa wanafunzi wanaohitimisha masomo yao katika taaluma mbalimbali.