Rais wa China akutana na mwenyekiti wa Chama cha United Russia
2022-12-21 17:28:34| cri

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC leo, hapa Beijing, amekutana na mwenyekiti wa Chama cha United Russia Bw. Dmitry Medvedev, ambaye yuko ziarani nchini China.

Rais Xi amemtaka Bw. Medvedev kuwasilisha salamu na matumaini mema kwa rais wa Russia Vladimir Putin, huku akisema kuwa mkutano mkuu wa 20 wa wajumbe wote wa CPC umeweka bayana jukumu la kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa yenye nguvu ya ujamaa na kuhimiza ustawi wa taifa la China kwa pande zote. Amesema, China ina imani kujiendeleza kwa njia ya usasa wa kichina, na kutoa fursa nyingi zaidi kwa amani na ustawi wa dunia.Ameongeza kuwa, CPC na Chama cha United Russia vimefanya mawasiliano kwa muda mrefu na vimekuwa njia na jukwaa pekee la kuimarisha uaminifu wa kisiasa kati ya China na Russia, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi mbili, kuonesha uratibu wa kimkakati wa nchi mbili, huku vikiunga mkono kwa dhati uhusiano kati ya China na Russia kuendelea kwa uvulivu katika zama mpya.

Bw. Medvedev amemkabidhi rais Xi barua iliyoandikwa na rais Putin, huku akiwasilisha salamu na matumaini mema ya rais Putin kwa rais Xi. Bw. Medvedev amempongeza rais Xi kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa CPC, huku akipongeza mkutano mkuu wa 20 wa CPC kupata maendeleo muhimu. Bw. Medvedev amesema, Maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wa CPC sio tu yamenufaisha watu bilioni 1.4 wa China, bali pia yana maana kubwa kwa dunia nzima, na anaamni kuwa sera na mipango iliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa 20 zitatekelezwa kwa ufanisi.