Mjumbe wa China akaribisha kupitishwa kwa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu DR Congo
2022-12-21 08:52:34| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun, amekaribisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kurejesha tena mamlaka ya tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na azimio la kuondoa matakwa ya kutoa taarifa ya usafirishaji wa silaha kwenda DRC.

Amesema kwa sasa, hali ya usalama mashariki mwa DRC bado ni mbaya, wakati makundi yenye silaha yakidhibiti maeneo makubwa na kutishia maisha na mali ya wakazi. Kutokana na hali ya sasa, kuhuishwa kwa mamlaka ya tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, kunafaa kwa amani na utulivu wa kikanda na kulingana na matarajio ya serikali ya DRC. Balozi Zhang amesema China imepiga kura kuunga mkono rasimu ya azimio hilo.

Balozi Zhang pia amesema China inatumai kwamba kwa kuendelea, Baraza la Usalama kwa kuzingatia mabadiliko ya hali, litarekebisha majukumu ya tume hiyo.