FAO yatahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Somalia
2022-12-21 09:17:04| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa onyo kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Somalia wakati maafa ya njaa yakiongezeka kwa kasi.

FAO imesema bado kuna wakati wa kubadilisha mwelekeo huo kwa kushughulikia mahitaji ya dharura ya jamii za vijijini ambazo ziko kwenye hatari kubwa zaidi.

Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Somalia Bw. Etienne Peterschmitt amesema misaada ya kibinadamu kwa nchi hiyo sasa inasaidia kuzuia matokeo mabaya kupita kiasi, lakini haitoshi kukomesha tishio la njaa linaloendeleakwa miezi kadhaa.

Uchambuzi wa Ukosefu wa Usalama wa Chakula uliotolewa hivi karibuni unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, umeonya kuwa watu wasiopungua laki 7.2 nchini humo wanaweza kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ifikapo mwezi Juni mwaka 2023.