Netanyahu wa Israel asema ameunda serikali ya muungano
2022-12-22 08:59:47| CRI

Waziri mkuu mteule wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa amefanikiwa kuunda serikali yake.

Dakika chache kabla ya muda wa mwisho wa saa sita usiku, ofisi ya Netanyahu ilisema katika taarifa kwamba Bw. Netanyahu alimpigia simu rais Isaac Herzog na kumfahamisha kwamba amefanikiwa kuunda serikali.

Chama cha Likud kinachoongozwa na Bw. Netanyahu bado hakijasaini makubaliano ya mwisho ya ushirikiano na washirika wake wanne kati ya watano, vyama vitatu vya siasa kali za mrengo wa kulia na vyama viwili vya Kiyahudi vya wahafidhina. Kwa mujibu wa sheria ya Israel, serikali mpya inatakiwa kuapishwa tarehe 2 Januari mwaka kesho.