Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 5.8 kwa mwaka huu
2022-12-22 08:58:56| CRI

Uchumi wa Kenya unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.8 kwa mwaka huu, ukiwa umepungua kutoka asilimia 7.5 ya mwaka 2021.

Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Kenya ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera ya Umma (KIPPRA) inasema ukuaji huo utasaidiwa na kurudi kwa matumizi na kutarajiwa kufufuka kwa sekta zote za uchumi.

Sekta ya kilimo inakadiriwa kukua kwa asilimia 2.3 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.2 kulikorekodiwa mwaka 2021 kutokana na ukame unaoshuhudiwa nchini Kenya.