Xi asisitiza kujenga nguvu ya China kwenye kilimo
2022-12-26 08:53:38| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuimarishwa juhudi za kujenga nguvu ya China kwenye kilimo na kufanya kazi nzuri katika shughuli za kilimo na maeneo ya vijijini.

Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano mkuu wa mwaka wa kazi za vijijini uliofanyika Ijumaa na Jumamosi hapa mjini Beijing.

Xi alibainisha kuwa kuendeleza ufufuaji wa maeneo ya vijijini kote nchini na kusonga kwa kasi ili kujenga nguvu ya China katika kilimo ni sehemu ya mipango ya kimkakati ya Kamati Kuu ya CPC ya kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kisasa ya ujamaa katika pande zote.

Aidha alitoa wito wa kuendeleza kazi zinazohusiana na kilimo, maeneo ya vijijini na wakulima na ufufuaji wa vijijini kama lengo, na kukuza kwa nguvu kilimo na vijiji vya kisasa.

Mkutano huo uliongozwa na Li Keqiang na pia kuhudhuriwa na Li Qiang, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi na Ding Xuexiang.