Idadi ya vifo kwenye mlipuko wa gesi nchini Afrika Kusini yafikia 15
2022-12-26 08:55:32| CRI


 

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Joe Phaalha jana alisema, idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa gesi uliotokea Boksburg nchini humo imeongezeka na kufikia 15 hadi jana asubuhi.

Jumamosi asubuhi, lori lililobeba gesi lilikwama chini ya daraja moja huko Boksburg, jimbo la Gauteng, na kusababisha moto na mlipuko.

Phaahla amesema, kwa jumla wagonjwa 24 na wafanyakazi 13 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Tambo ambayo ipo mita 100 kutoka eneo la tukio, walijeruhiwa. Miongoni mwa wafanyakazi waliojeruhiwa, dereva na wauguzi wawili wamefariki dunia.