Watu milioni 100 wakimbia makazi yao duniani mwaka 2022
2022-12-27 09:34:15| CRI


 

Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Jumatatu lilisema watu milioni mia moja kote duniani walilazimika kukimbia makazi yao katika mwaka huu wa 2022, wakati huohuo UM unaendelea kusaidia wale wenye mahitaji kwa njia nyingi.

Mkuu wa shirika hilo, Filippo Grandi, alielezea idadi hiyo kama "rekodi isiyopaswa kuwekwa,". Idadi hiyo imeongezeka kutoka milioni 90 mwaka 2021. Kuzuka kwa vurugu, au migogoro ya muda mrefu, ndio sababu kuu za uhamiaji katika sehemu nyingi za dunia, ikiwa ni pamoja na Ukraine, Ethiopia, Burkina Faso, Syria na Myanmar.

UM umeonya kuwa maelfu ya wahamiaji waliokata tamaa waliichukulia Ulaya kama eneo lao la kukimbilia, wakiweka maisha yao mikononi mwa wafanya magendo ya binadamu, na kuanza safari za hatari kuvuka bahari ya Mediterania.