Rais wa China asisitiza kuhakikisha kihalisi usalama wa maisha na afya ya umma
2022-12-27 10:45:02| cri

Wakati wa kuadhimisha miaka 70 ya harakati za afya za kitaifa, rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, hivi sasa China inakabiliwa na hali mpya na majukumu mapya katika kudhibiti na kukinga janga la COVID-19, na ni lazima kuendeleza harakati za afya za kitaifa kwa mujibu wa malengo zaidi.

Pia amesisitiza kuwa inapaswa kuwaongoza raia kupata elimu ya afya, kujua uwezo wa afya, kuwa na mienendo mizuri ya kiafya, kuishi kwa njia ya kiafya, na kuhakikisha kihalisi usalama wa maisha na afya ya umma.