China kusimamia COVID-19 kwa kuchukua hatua dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ya daraja B
2022-12-27 09:34:51| CRI


 

China itasimamia COVID-19 kwa kuchukua hatua dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ya daraja B, badala ya magonjwa ya kuambukiza ya daraja A, katika mabadiliko makubwa ya sera zake za kukabiliana na janga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu na Idara ya Kitaifa ya Afya, kuanzia Januari 8, China itashusha udhibiti wa ugonjwa huo kutoka Daraja A hadi B kulingana na sheria ya nchi ya kuzuia na kutibu magonjwa ya kuambukiza, na kuuondoa katika udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza unaofanywa kwa mujibu wa Sheria ya Afya na karantini ya Jamhuri ya Watu wa China.

Hivi sasa, COVID-19 imeainishwa kama ugonjwa wa kuambukiza wa Daraja B lakini unategemea hatua za kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kuambukiza wa Daraja A nchini China. Taarifa pia imesema mamlaka itaondoa hatua za kuwaweka watu karantini walioambukizwa virusi vya corona na kuacha kufuatilia watu waliokuwa karibu nao ama kutaja maeneo yenye hatari kubwa na hatari ndogo.