Ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” wapata mafanikio makubwa katika mwaka 2022
2022-12-27 09:36:03| CRI


 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amesema mwaka huu ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeendelea kupiga hatua, na kupata mafanikio mbalimbali.

Kipindi cha kwanza cha mradi wa reli ya Logos nchini Nigeria inayojengwa na kampuni ya China kimemalizika kwa mafanikio, ambapo reli hiyo itakuwa reli nyepesi ya kwanza ya umeme katika kanda ya Afrika magharibi. Akijibu swali kuhusu mradi huo Mao amesema utapunguza shinikizo la barabarani mjini Lagos kwa kiasi kikubwa, na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa Nigeria, na pia utatoa uzoefu katika ujenzi wa reli nchini humo na hata kanda nzima ya Afrika magharibi.

Mao amesema ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umekuwa injini mpya wa maendeleo ya nchi mbalimbali, na kukaribishwa na watu wa nchi hizo. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na pande nyingine husika kujumuisha uzoefu na kutunga mipango mipya, ili kulifanya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilete ustawi zaidi duniani.