Watu 2 wauawa katika shambulizi linalosadikiwa kufanywa na kundi la al-Shabab nchini Kenya
2022-12-27 08:35:28| cri

Watu wawili juzi walipigwa risasi na kuuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la al-Shabab katika mji wa Lamu uliopo mkoa wa pwani nchini Kenya.

Mkuu wa mkoa wa pwani Bw. John Elungata alisema, nyumba kadhaa katika eneo hilo pia zilichomwa moto na washambuliaji katika eneo la Pandaguo. Washambuliaji hao walifukuzwa na askari wa akiba baada ya mapigano makali ya risasi.