Katibu Mkuu wa UM atoa angalizo duniani katika Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha na Magonjwa ya Mlipuko
2022-12-28 08:46:00| CRI


 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumanne alitoa angalizo duniani katika Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha na Magonjwa ya Mlipuko, ambayo huadhimishwa Disemba 27 kila mwaka.

Katika ujumbe wake kwa ajili ya siku hiyo ya kimataifa, Guterres alisema dunia lazima iungane, ambapo ugonjwa wa UVIKO-19 ulikuwa wito wa kutanabahisha watu. Ameongeza kuwa gharama zimekuwa kubwa sana na kubainisha kwamba tangu janga hilo litokee, mamilioni ya maisha yamepotea, na mamia ya mamilioni ya watu wameugua, uchumi umedidimia, mifumo ya afya imedhoofika, na matrilioni ya dola kupotea.

Mbali na hapo, amesema hatua za kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu zimetupiliwa mbali, huku nchi zinazoendelea mara nyingi ziliachwa zijitegemee, zilinyimwa chanjo, vipimo au matibabu waliyohitaji kulinda watu wao bila ya aibu. Bw. Guterres ameonya kuwa

UVIKO-19 halitakuwa janga la mwisho kuwakabili binadamu.