Dhoruba za msimu wa baridi nchini Marekani zaua watu 57
2022-12-28 08:43:16| cri

Idadi ya vifo kutokana na dhoruba za msimu wa baridi nchini Marekani imefikia 57, huku idadi ya vifo kutokana na dhoruba za theluji katika jimbo la New York Magharibi ikiongezeka kwa kiasi kikubwa. Rais wa Marekani Joe Biden ameamuru mashirika ya serikali kuu kusaidia serikali za majimbo.

Gavana wa jimbo la New York Bibi Cathy Hochul jana alisema kwamba mazingira ya nje bado ni hatari. Theluji imeanza kuanguka tena, na ni mapema sana kutangaza kwamba dhoruba ya theluji imekwisha.