Rais wa China atoa hotuba muhimu katika mkutano wa Kamati Kuu ya CPC
2022-12-28 15:31:24| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wa kidemokrasia unaolenga kukosoa na kujikosoa, ili kutekeleza kikamilifu fikra ya rais wa China Xi Jinping ya ujamaa wenye umaalumu wa kichina katika zama mpy.
Mkutano huo unalenga kuongoza wanachama na makada wa chama kutekeleza mipango muhimu iliyotolewa katika Mkutano wa Mkuu wa 20 wa CPC, kushikilia na kuimarisha uongozi wa pande zote wa CPC, kushikilia wazo la maendeleo linalowalenga wananchi, kusimamia kwa makini mambo ya chama, kutekeleza kwa pande zote majukumu ya kisiasa, kuhitimisha mafanikio yaliyopatikana na pia kujikosoa juu ya mapungufu yaliyopo.
Rais Xi ametoa hotuba muhimu katika mkutano huo akisisitiza kuwa, utekelezaji wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ni kazi kuu ya kisiasa kwa chama kizima kwa sasa na kipindi kijacho. Amesema wajumbe wote wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ni lazima waongoze katika kuelewa kwa kina na kutekeleza kikamilifu maamuzi mbalimbali yaliyotolewa kwenye mkutano huo.