Mkutano wa mwaka 2022 wa waanzilishi wa BRSN wafanyika
2022-12-28 08:43:55| CRI


 

Mwenyekiti wa Baraza la Waanzilishi wa Mtandao wa Utafiti wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRSN) Fu Hua amesema, katika miaka 10 iliyopita, pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limeendelea kusukumwa mbele na kupata matokeo madhubuti, na limetoa mchango mkubwa kwa maendeleo duniani .

Fu amesema hayo kwenye mkutano wa mwaka 2022 wa BRSN uliofanyika jana. Amebainisha kuwa jamii ya kimataifa ina matarajio makubwa kwa maendeleo ya hali ya juu ya ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na ikiwa jopo la washauri bingwa, BRSN inapaswa kutekeleza majukumu yake ya kuhimiza mchakato wa ujenzi huo, na kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa nchi husika.