Watu 7 wafariki katika ajali ya gari iliyovamia watu kusini mwa Nigeria
2022-12-29 08:52:01| cri

Watu saba walifariki na wengine 29 kujeruhiwa baada ya dereva kushindwa kulidhibiti gari lake na kuvamia na kugonga umati wa watu kwenye kanivali katika jimbo la Cross River kusini mwa Nigeria siku ya Jumanne.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha jimbo la Cross River, Bw. Maikano Hassan, alisema watu hao saba walikufa hapohapo kwenye eneo la ajali na majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya eneo hilo kwa matibabu, ambapo shughuli za kanivali katika siku hiyo zilisitishwa baada ya tukio hilo.