Ukumbi wa Wanawake-Haki za mwanamke na msichana
2022-12-29 10:47:38| CRI

Siku ya Haki za Binadamu huadhimishwa duniani kote tarehe 10 Desemba kila mwaka. Tarehe hiyo ilichaguliwa kwa heshima na kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tarehe 10 Desemba 1948, kwenye Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (UDHR). Azimio la kwanza la kimataifa la haki za binadamu ni moja ya mafanikio makubwa ya Umoja wa Mataifa. Kaulimbiu ya Siku ya Haki za Kibinadamu kwa mwaka 2022 ni Utu, Uhuru na Haki kwa Wote. Azimio na Katiba ya WHO zote mbili zinadai kuwa afya ni haki ya msingi ya binadamu kwa watu wote.

Haki za binadamu limekuwa ni suala ambalo linatesa wengi, ingawa kuna kampeni nyingi zinazoendeshwa na wanaharakati wanaotetea haki za binadamu, na kutengwa siku kama hii lakini dunia bado inashuhudiwa haki hizi zikikiukwa kwa makundi mbalimbali, likiwemo kundi la wanawake na watoto wa kike. Hivyo ikiwa hivi majuzi tu tumetoka kuadhimisha haki za binadamu duniani, leo kwenye kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake tutaangalia tunaangalia jinsi wanawake na wasichana wasivyotimiziwa haki zao.