Benki za China Afrika zaendelea kupongezwa kwa kuchangia maendeleo ya kiuchumi
2022-12-29 10:42:50| CRI

Kipindi cha Daraja kinachokujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kinakufahamisha mambo mbalimbali kuhusu uhusiano, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha leo, licha ya habari za wiki hii zilizohusisha China pamoja na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti kuhusu Benki za China Afrika kuendelea kupongezwa kwa kuchangia maendeleo ya kiuchumi, pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi.