China yapinga vyombo vya habari vya magharibi kuchafua rekebisho la sera ya China ya kudhibiti na kukinga janga la COVID-19
2022-12-29 08:55:13| CRI


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China jana kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi vinachafua rekebisho la sera ya China ya kudhibiti na kukinga janga la COVID-19, hatua hii haiambatani na ukweli.

Bw. Wang amesema, tangu mlipuko wa janga hilo utokee miaka mitatu iliyopita, serikali ya China siku zote inashikilia kuweka kipaumbele wananchi na maisha yao. Viwango vya idadi ya magonjwa mabaya na vifo nchini China vyote ni vya chini zaidi vikilinganishwa na dunia kote.