IOM yasema zaidi ya wahamiaji 100,000 wa Ethiopia warejea nyumbani katika miezi 10 ya kwanza
2022-12-30 09:11:41| CRI


 

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema zaidi ya wahamiaji 100,000 wa Ethiopia wamerejea nyumbani kutoka nchi za nje katika kipindi cha miezi kumi ya kwanza ya 2022.

Katika Mpango wake mpya wa Kukabiliana na Mgogoro wa Ethiopia uliotolewa Jumatano shirika hilo lilisema, kati ya Januari na Oktoba 2022, IOM ilisajili zaidi ya wahamiaji 100,000 wanaorejea Ethiopia, ambapo wengi wao zaidi ya 71,000 wakitoka Saudi Arabia. IOM liliongeza kuwa idadi ya kutisha ya wahamiaji wamefika wakiwa maskini na hali mbaya ya kiafya na kiakili, mambo ambayo yanaleta changamoto kwa uwezo wa nchi mwenyeji.

Kwa mujibu wa IOM takriban theluthi moja ya wahamiaji wote waliorejea kutoka Saudi Arabia wanatoka katika maeneo yaliyoharibiwa na migogoro.