Timu ya matibabu ya China nchini Sudan yaandaa warsha ya kitengo cha wagonjwa mahututi
2022-12-30 09:10:38| CRI


 

Timu ya madaktari wa China nchini Sudan Alhamisi iliandaa warsha ya mafunzo ya kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya mjini Khartoum kama njia ya kuimarisha ubadilishanaji wa teknolojia ya matibabu kati ya nchi hizi mbili.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa timu ya 37 ya madaktari wa China nchini Sudan, Xing Zhijing, warsha hiyo iliyofanyika katika Hospitali ya Urafiki ya Omdurman ilijumuisha mihadhara ya kuboresha ujuzi wa hospitali hiyo ili kujiandaa kwa ajili ya kuanzishwa kwa kitengo cha wagonjwa mahututi.

Guo Hu, kansela wa mamabo ya kibiashara katika Ubalozi wa China nchini Sudan, alisisitiza kuwa historia ndefu ya mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wa kimatibabu kati ya China na Sudan ni mfano bora wa urafiki wa kina.

Naye Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Nchi Mbili na Kimataifa ya Kurugenzi ya Afya ya Kimataifa katika Wizara ya Afya ya Sudan, Shahd Osman, ameshukuru sana juhudi za China katika kuimarisha mfumo wa afya wa Sudan.