Rais Xi Jinping wa China atoa pongezi kwa rais Cyril Ramaphosa kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa ANC
2022-12-31 19:36:53| cri

Tarehe 31 Desemba Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini humo cha African National Congress (ANC), na kumtakia kupata mafanikio makubwa zaidi katika kazi yake.

Rais Xi Jinping amesema, Chama cha Kikomunisti cha China na Chama cha ANC vina urafiki mkubwa wa jadi, ushikiano kati ya vyama viwili umepata mafanikio mengi, na vimetoa mchango mkubwa kwa kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili. Anapenda kushirikiana na rais Cyril Ramaphosa, kuendeleza uhusiano kati ya vyama viwili, na kujenga jumuiya ya China na Afrika na jumuiya ya kimataifa yenye mustakabali wa pamoja.