Utalii wa Afrika Kusini waonyesha dalili za kufufuka katika kipindi cha sikukuu
2022-01-03 08:40:30| CRI

Meya wa mji wa Cape Town wa Afrika Kusini Bw. Mxolis Kaunda, amesema utalii wa Afrika Kusini umeonyesha dalili za kufufuka wakati hoteli za mji wa pwani wa Durban zikijaa kwa asilimia 80, na mji huo kupokea watalii laki 2 kwenye msimu wa sikukuu.

Bw. Kaunda amesema walipenda kuwa na matokeo hayo kwa sababu mji huo uliathiriwa sana na janga la COVID-19 na watu wengi walipoteza ajira zao. Amesema takwimu hizo zinaonyesha kuwa wanafanya kazi nzuri. Amesema katika kipindi cha sikukuu migahawa ilijaa watalii.

Katika wikiendi ya krismas pekee, watu laki mbili walitembelea mji wa Cape Town na kutumia karibu dola milioni 10, na mchango wake kwa pato la mji huo ulikuwa Rand milioni 350.

Siku ya Alhamisi Afrika Kusini iliondoa marufuku ya kutoka nje usiku.