Mtu mmoja akamatwa kufuatia ajali ya moto kwenye bunge la Afrika Kusini
2022-01-03 08:41:08| CRI

Waziri wa ujenzi na miundo mbinu wa Afrika Kusini Bibi Patricia De Lille amesema mtu mmoja amekamatwa kufuatia ajali ya moto uliotokea jana kwenye bunge la Afrika Kusini.

Mtu huyo alikamatwa ndani ya jengo la bunge na sasa amekabidhiwa kwa Kurugenzi ya Polisi ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai, Hawks.

Jengo la zamani la bunge hilo na la baraza la chini lilikuwa linawaka moto tangu alfajiri ya jana, lakini chanzo cha moto huo bado hakijulikani.

Idara ya zima moto ya mji wa Cape Town ilipigiwa simu na kufika kwenye eneo la tukio baada ya dakika sita.

Rais Cyril Ramaphosa ameahidi uchunguzi wa kina kuhusu moto huo na kuangalia ni hatua gani zinatakiwa kuchukuliwa.