Watu 8 wafariki katika ajali ya barabarani magharibi mwa Kenya
2022-01-03 09:08:25| CRI

Polisi nchini Kenya wamesema watu wanane walifariki papo hapo baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kuligonga lori moja lililokuwa limesimama katika barabara kuu kati ya Webuye hadi Eldoret jana Jumapili.

Kamanda wa polisi katika eneo la Magharibi Bi. Peris Kimani, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea saa 11 alfajiri, na kusema matatu hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Bungoma kuelekea Nairobi kupitia barabara kuu ya Webuye-Eldoret.

Kwa mujibu wa polisi ajali mbaya ni jambo la kawaida nchini Kenya kutokana na kuendesha gari kwa uzembe, kuendesha gari dereva akiwa amelewa, wenda kwa miguu wakiwa wamelewa, waendesha pikipiki kulewa na kutovaa helmeti.