Wanajeshi wanne wauawa katika mashambulizi ya makombora ya Houthi nchini Yemen
2022-01-03 09:15:35| cri

Wanajeshi wasiopungua wanne wa kikosi kinachounga mkono serikali ya Yemen wameuawa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na kundi la Houthi Jumapili iliyopita katika jimbo la Shabwa, kusini mwa nchi hiyo.

Ofisa mmoja wa jeshi alisema kombora lililofyatuliwa na upande wa Houthi limeshambulia soko moja la umma na kituo cha mafuta katika eneo la Usaylan. Habari zinasema mapigano kati ya jeshi la serikali ya Yemen linaloungwa mkono na jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia na wapiganaji wa Houthi bado yanaendelea katika sehemu mbalimbali za jimbo hilo lenye raslimali ya mafuta. Na jeshi la serikali limepata maendeleo kwenye mapigano hayo katika saa zilizopita ambapo kundi la Houthi limepoteza maeneo yake ya Usaylan.

Yemen imeshuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 2014, tangu kundi la Houthi lilipoiteka sehemu kubwa ya nchi hiyo.