Syria yapokea dozi milioni 1 za chanjo za COVID-19 kutoka China
2022-01-04 09:08:25| cri

Wizara ya Afya ya Syria imepokea shehena ya dozi milioni moja za chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China Jumatatu wiki hii. Waziri wa wizara hiyo Bw. Hasan al-Ghabash na balozi wa China nchini Syria Bw. Feng Biao walihudhuria sherehe ya makabidhiano mjini Damascus.

Bw. al-Ghabash alisema msaada kutoka China umechangia katika mambo ya afya nchini humo na kukabiliana na janga la COVID-19, na kuhimiza mchakato wa utoaji wa chanjo. Kwa upande wa Balozi Feng Biao alitoa wito kwa ushirikiano na mshikamano zaidi wa jumuiya ya kimataifa wakati janga la COVID-19 likiendelea.

China imetoa msaada wa chanjo mara kadhaa kwa wizara ya afya ya Syria, ambayo imeanzisha kampeni ya utoaji wa chanjo kote nchini ikitarajia kupunguza idadi ya maambukizi.