Kenya yaanza kutoa dozi ya ziada ya chanjo ya Covid-19 kwa wananchi wake
2022-01-05 08:42:59| CRI

Wakenya ambao wamepata dozi kamili za chanjo ya COVID-19 wameitikia wito wa kupokea dozi ya ziada wakati nchi hiyo inashuhudia wimbi la maambukizi ya virusi vilivyobadilika aina ya Omicron.

Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe amesema, Kenya imeanza kutoa dozi ya tatu ya chanjo kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 55, wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele na maofisa wa usalama kuanzia Januari 1, ambapo watu 18,000 wamepokea dozi hiyo ya ziada.