Rais wa China afanya ukaguzi wa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
2022-01-05 08:43:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Jumanne alifanya ukaguzi wa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.

Rais Xi alitembelea uwanja wa taifa wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu, kituo kikuu cha habari, kijiji cha wanamichezo, kituo cha uongozi wa operesheni za michezo na kambi ya mafunzo ya michezo ya majira ya baridi, akikagua hali ya maandalizi ya michezo hiyo na utayari wa wanamichezo wa China kwa ajili ya michezo hiyo.

Rais Xi ametoa salamu za mwaka mpya kwa wanamichezo, makocha, watu wanaojitolea na wajumbe wa timu za operesheni, vyombo vya habari na watafiti wa sayansi.