WHO bado linapendekeza karantini ya siku 14 kwa walioambukizwa COVID-19
2022-01-05 09:05:48| CRI

Pamoja na kuwa watu wanaweza kupata nafuu ndani ya siku tano na siku saba tangu walioambukizwa COVID-19, Shirika la Afya Duniani WHO bado linapendekeza karantini ya siku 14.

Ofisa wa WHO Bw. Abdi Mahamud amesema nchi mbalimbali zinaweza kufanya uamuzi kuhusu muda wa kukaa karantini. Amesema kwenye nchi zenye maambukizi machache, karantini ya muda mrefu inaweza kusaidia kufanya maambukizi yawe ya chini sana. Lakini kwenye maambukizi ya watu wenye umri wa chini, karantini za muda mfupi zinaweza kukubalika ili kufanya mambo yaendelee katika hali ya kawaida.

Ofisa huyo pia amesema kuna uwezekano wa mtu kuambukizwa mafua na COVID-19 kwa pamoja, lakini kwa kuwa virusi vinashambulia mwili kwa njia tofauti, kuna “hatari kidogo” kwa virusi hivyo kuungana na kuwa kirusi kipya.