Watu 10 wafa katika ajali ya boti Zanzibar
2022-01-06 09:17:56| CRI

Kamanda wa polisi wa mkoa wa kusini wa Pemba Bw. Richard Mchomvu amesema takriban watu 10 wamefariki katika ajali ya kuzama kwa boti iliyokuwa ikisafirisha waombolezaji jumanne jioni huko Zanzibar na wengine 15 wameokolewa.

Amesema boti hiyo iliyokuwa ikisafirisha waombolezaji kutoka Chakechake kuelekea kisiwa cha Panza kuhudhuria mazishi ya jamaa yao, ilipinduka baharini saa 12 jioni kwa saa za huko.

Pia Bw. Mchomvu amesema shughuli za uokoaji zilizoongozwa na kikosi cha kupambana na magendo na wakazi wa eneo hilo wakiwemo wavuvi, zilikwamishwa na mawimbi na giza.