Sheria zalinda haki na maslahi ya wanawake
2022-01-06 14:11:48| CRI

Hivi karibuni China ilifanya marekebisho ya sheria mbalimbali zinalenga kulinda haki za wanawake, kuondoa vitendo vinavyowatenga wanawake na kuimarisha hisia zao za kujihisi ni salama. Nchi mbalimbali zimetunga sheria za kulinda haki za wanawake na kuhakikisha wako salama, lakini mara nyingi haki hizo hukiukwa na wanaofanya hivyo kutochukuliwa hatua zozote. Kutokana na hilo, China imeamua kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusu haki za wanawake na kuhakikisha haki hizo zinasimamiwa na kutekelezwa kikamilifu. 

Na katika kipindi cha leo, tutazungumzia kuhusu haki za wanawake kuhusu unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi katika sehemu za kazi.