Rais Xi Jinping wa China apinga vikali jaribio lolote la kuiyumbisha Kazakhstan
2022-01-07 21:44:57| cri

Rais Xi Jinping alisema wa China leo amesema China inapinga vikali kundi lolote linalojaribu kudhoofisha utulivu wa Kazakhstan, kutishia usalama wa nchi hiyo, na kuhujumu maisha ya amani ya watu wa nchini hiyo. Katika ujumbe wa maneno kwa Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, Rais Xi amesema China inapinga vikali jaribio lolote la majeshi ya nje ya kuzusha machafuko na kuanzisha "mapinduzi ya rangi" huko Kazakhstan, pamoja na jaribio lolote la kuharibu urafiki kati ya China na Kazakhstan na kuvuruga ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.