Waziri wa mambo ya nje wa China afafanua malengo matatu ya ziara yake barani Afrika
2022-01-07 09:01:06| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi ameweka wazi malengo matatu ya ziara yake barani Afrika alipokutana na mwenzake wa Kenya Bibi Raychelle Omamo huko Mombasa, Kenya.

Wakati wa mazungumzo hayo, Bw. Wang amesema desturi ya China kufanya ziara ya kwanza barani Afrika katika mwanzo wa mwaka mpya sasa imedumishwa kwa miaka 32. Desturi hiyo imeonesha China inathamini urafiki kati yake na Afrika, kutanguliza Afrika katika mambo ya diplomasia ya China, na pia inatumai kuwa rafiki na mwenzi mzuri wa Afrika.

Akitaja malengo matatu ya ziara yake hii barani Afrika, amesema ni kushirikiana na Afrika kushinda janga la COVID-19, kuharakisha utekelezaji wa matokeo yaliyopatikana katika Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na kulinda maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili.