Biden ataka shambulizi la Januari 6 katika jengo la bunge la Marekani kamwe halitatokea tena
2022-01-07 09:02:49| cri

Rais Joe Biden wa Marekani amesema Wamarekani wanatakiwa kuhakikisha kuwa shambulizi kama lililotokea katika jengo la bunge la Marekani mwaka mmoja uliopita “kamwe halitatokea tena”, ambalo limeonesha mpasuko mkubwa katika jamii ya nchi hiyo.

Biden alisema hayo Alhamisi katika hotuba yake aliyoitoa Ukumbi wa Statuary nje ya jengo la Bunge ili kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu jengo hilo lilipovamiwa. Amesema siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita katika eneo hili takatifu, demokrasia ilishambuliwa, azma ya watu ilishambuliwa, na Katiba ya Marekani ilikabiliwa na vitisho vikubwa.

Biden pia alimshutumu mtangulizi wake Donald Trump kwa kueneza "mtandao wa uwongo" kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ambao uliweka msingi wa shambulio katika bunge mwaka mmoja uliopita, akisema madaraka ya urais na lengo lake ni kuunganisha taifa, na sio kuligawanya, ni kuinua watu, na sio kuwatenganisha watu.