Waziri wa Mambo ya Nje ya China afafanua pendekezo la maendeleo ya amani kwa Pembe ya Afrrika
2022-01-07 15:13:39| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi amesema China iko tayari kutoa ‘Pendekezo la Maendeleo ya Amani katika Pembe ya Afrika’ ili kuunga mkono nchi za kanda hiyo katika kukabiliana na changamoto za usalama, maendeleo na uongozi.

Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi baada ya kufanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya Bi. Raychelle Omamo, Wang Yi amefafanua mtazamo wa China kuhusu hali ya sasa katika Pembe ya Afrika. Amesema China iko tayari kutoa pendekezo hilo ili kuunga mkono kanda hiyo kutimiza utulivu, amani na ustawi wa kudumu.

Wakati huohuo, Wang Yi amesema kile kinachoitwa ‘mtego wa madeni’ hakina msingi wowote na ni jambo lililobuniwa na watu wanaotaka kuchafua uhusiano wa China na Afrika.

Amesema ushirikiano wa China na Afrika ni wa Kusini na Kusini, ukionyesha kuungana mkono na kusaidiana kati ya nchi zinazoendelea, na kuongeza kuwa China haijawahi kuweka masharti ya kisiasa katika ushirikiano wake na Afrika, na pia China haijawahi kulazimisha matakwa yake kwa nchi nyingine.