Katibu mkuu wa UM azitaka pande zote za Kazakhstan zitulie
2022-01-07 09:00:29| cri

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric jana alisema Antonio Guterres amezitaka pande zote za Kazakhstan ziepuke vurugu na kuhimiza mazungumzo ili kukabiliana na hali ya kukosekana utulivu.

Stephane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Kazakhstan, pia umefanya mawasiliano kwa mara kadhaa na mamlaka ya sasa ya Kazakhstan, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya jana asubuhi kwa njia ya simu kati ya mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa UM anayeshughulikia suala la Asia ya Kati Natalia Gherman na naibu waziri wa mambo ya nje wa Kazakhstan Akan Rakhmetullin. Kwenye mazungumzo yao, Natalia Gherman amesisitiza tena pande zote husika ziwe na uvumilivu, kuepuka vurugu, na kuhimiza mazungumzo ili kukabiliana na hali ya sasa.