Watu 19 wafariki katika ajali mbaya ya moto mjini New York
2022-01-10 08:33:49| CRI

Watu 19 wamefariki wakiwemo watoto tisa katika ajali mbaya ya moto iliyotokea kwenye jengo la makazi ya watu lililoko Bronx, mjini New York, Marekani, jana jumapili.

Akithibitisha ajali hiyo, Meya wa Mji wa New York Eric Adams ameeleza kusikitishwa na vifo vilivyotokana na ajali hiyo, na kuwashukuru askari wa zimamoto kwa kufanikiwa kudhibiti moto huo.

Amesema watu 32, tisa wakiwa wamejeruhiwa vibaya, wamepelekwa hospitali, na wengine 22 walipata majeraha madogo.