Takriban watu 5,800 wakamatwa kwenye ghasia nchini Kazakhstan
2022-01-10 08:32:16| cri

 

 

Ofisi ya mawasiliano ya Ikulu nchini Kazakhstan jana imesema, takriban watu 5,800 wamekamatwa kwenye ghasia nchini humo, wakiwemo raia kadhaa wa kigeni.

Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo imesema, hivi sasa utulivu umerejea katika sehemu mbalimbali nchini Kazakhstan, na uendeshaji wa huduma za umma na mifumo ya msaada wa maisha unarejeshwa.

Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev amesisitiza imani yake ya kurejesha kikamilifu utaratibu na usalama wa nchi hiyo.