Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa FOCAC
2022-01-10 09:06:19| CRI

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa FOCAC_fororder_src=http___world.chinadaily.com.cn_img_attachement_png_site1_20150914_448a5bd66c7d1760fd2712.png&refer=http___world.chinadaily.com

Mjumbe wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Xu Jinghu amesema, ziara ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi katika nchi za Eritrea, Kenya na Comoro barani Afrika itaharakisha utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika hivi karibuni nchini Senegal.

Xu amesema, katika miaka zaidi ya 20 tangu kuanzishwa kwa FOCAC, China imejenga miundombinu mingi barani Afrika, ikiwemo viwanja vya ndege, bandari, reli, barabara, na vituo vya umeme, na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii barani humo. Ameongeza kuwa, hatua mpya za ushirikiano kati ya China na Afrika, ikiwemo “Miradi Tisa” iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa FOCAC uliofanyika nchini Senegal, na Mpango wa mwaka 2035 wa Ushirikiano kati ya China na Afrika zilitungwa kwa kuendana na hali mpya ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na kuharakisha utekelezaji wa hatua hizo ni lengo muhimu la ziara hiyo ya Wang.